Jumamosi ya March 24 2018 mashindano ya Rugby kwa mara ya pili mfululizo yalifanyika jijini Dar es Salaam katika shule ya kimataifa ya Tanganyika na kushirikisha shule za msingi zaidi ya 10 za mkoa wa Dar es Salaam.
Mashindano hayo ambayo yamefanyika kwa mara ya pili mfululizo na kupata muitikio mkubwa licha ya kuwa mchezo wa Rugby kwa Tanzania sio maarufu sana ukilinganisha na soka, yamemalizika kwa kushuhudia shule ya Ananasifu kuibuka Mabingwa wa mchezo huo.
Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na G4S kwa kuleta waalimu kutoka nje ya nchi kuhakikisha watoto wanaelewa sheria za mchezo huo yamemalizika kwa timu za shule ya msingi kushika na pili na shule ya msingi Victoria kumaliza nafasi ya tatu.
EXCLUSIVE: Kingine usichokifahamu kutoka kwa Victor Wanyama wa Tottenham