Miezi michache ilyopita club ya Yanga kupitia kwa mkuu wake wa idara ya habari na mawasiliano Dismas Ten walitangaza kuanzisha jarida la club hiyo litakalokuwa linapatikana mitaani kila baada ya miezi mitatu.
Kutengenezwa kwa jarida hilo kuliwafanya waandishi na watu mbalimbali waipongeze Yanga na kumkosoa afisa habari wa Simba Haji Manara kuwa yeye kama mkuu wa idara ya habari na mawasiliano ameshindwa kufanya kitu kama hicho kwa Simba.
Jarida la Yanga kwa sasa limetoweka mtaani na waandishi walipomuuliza katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa akaeleza kuwa wameacha kutoa jarida hilo kutokana na kukosa wateja kutokana na kuliuza Tsh 3000, sasa leo Haji Manara kaandika hivi kwa waliomkosoa.
“Kiko wapi? wazaramo twasema Zilongwa mbali na Zitendwa mbali…nilidhihakiwa kwa mbwembwe kubwa..nikaandikiwa makala na baadhi ya waandishi…mimi nilijibu nina uzoefu mkubwa kwenye taaluma na Soka la nchi hii”
“Sikurupuki ili tu kuonekana mweledi..nilitoa miezi sita kama litadumu..haijafika hata minne…naambiwa issue namba moja imeuza copy sabini na mbili tu, Hahahahaha 😁😁nacheka kwa dharauuuuuuu….kudadadeki bin shubamit”
Hivi ndio Simba walivyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Al Masry