Jengo la Kitega Uchumi la Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro lililopo jijini Arusha ambalo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi June mwaka huu litakuwa kivutio cha kihistoria cha utoaji wa huduma za utalii nchini.
Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla muda mfupi baada ya kukagua jengo hilo ambalo linasemekana kuwa refu kuliko majengo yote jijini humo likiwa na jumla ya ghorofa 18.
“Tutapamba pia jengo hili na” live screen” (Mabango ya Video Mubashara) za vivutio, hivyo wanyama wakiwa wanapita huko porini watakuwa wanaonekana “LIVE” (Mubashara) kwenye jengo hili kupitia LED Screen ambazo zitakuwa zimezunguka jengo hili” -Dk. Kigwangalla.
Atakachokifanya Mtoto Anthony akipata Mshahara wake wa kwanza