Kulikuwa na taarifa ambayo imesambaa mitandaoni kuhusu ishu ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Moses Nnauye kutangaza kuhusu kupigwa marufuku baadhi ya aina ya mavazi kwa wanawake na wanaume… taarifa hiyo ikaenda mbali na kutaja faini ya 100,000/= kwa atakayekiuka.
Taarifa kutoka kwenye habari ya Clouds TV imempata Waziri Nape Nnauye >>> “Taarifa hiyo sio ya kweli ni taarifa ambayo imetungwa… Wizara hatuna website kama hiyo na hatujawahi kuzungumza jambo hilo. Nadhani ni watu wabaya wasiokuwa na nia njema ambao huenda nia yao ilikuwa ni kuichafua Wizara pamoja na Waziri. Hiyo sio habari ya kweli, ni uzushi” >>- Waziri Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa Wizaya hiyo amesema ishu haijaishia hapohapo kuwacha aliyetunga uzushi huo >>> “Tayari kuna Sheria ya Mitandao ya mwaka 2015, itatumika vizuri kuhakikisha uzembe huo unakomeshwa… popote anaposikia ni vyema akajisalimisha mwenyewe, mkono wa Sheria utamfikia popote alipo na atakamatwa“>>> Katibu Mkuu, Prof. Elisante Ole Gabriel.
Sauti ya stori hii hapa niliyokurekodia habari ya Clouds TV.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE