Wakati mamlaka zikitafuta mbinu mbalimbali za kudhibiti matumizi ya maji, Kijana wa Kitanzania, Gibson Kawago amefanya ubunifu wa kutengeneza Pampu ya Maji inayotumia kadi ili kudhibiti matumizi ya maji
Kawago amesema alianza masuala ya utengenezaji wa vifaa vya umeme tangu akiwa mdogo ambapo wazazi wake walikuwa wakimkataza lakini aliendelea kufanya hivyo hadi pale walipoamua kumpeleka shule.
Amesema ametengeza mfumo wa Solar Water Pump kwa kutumia kadi ili kudhibiti matumizi ya maji na kwa mara ya kwanza aliuanza kutengeneza Desemba 2018 ambapo anasema mfumo huo hajauchukua sehemu bali ni ubunifu wake.
“Mtu anayefanya umwagiliaji huko vijijini anampa mtu mmoja kwa ajili ya kutumia maji na sio kila mtu, hivyo hata ukiasha haiwaki hadi uwe na kadi, hivyo inamsaidia kudhibiti maji,”amesema.