Nchi nyingi za Afrika hususani zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara zinaendelea kukabiliana na tatizo la ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu haswa haswa kwa watu wenye tatizo la ulemavu wa ngozi huku jitihada mbalimbali zikifanyika kutokomeza hali hiyo.
Katika jitihada hio nchi Zimbabwe kwa mara ya kwanza, binti mwenye ulemavu wa ngozi Sithembiso Mutukura ametwaa taji la urembo kwenye shindano la urembo kwa mabinti wenye ulemavu wa ngozi.
Shindano hili linaelezwa kulenga kupingana na dhana potofu juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ili kuwafanya wapate haki zao zote za msingi.
BREAKING: Alichozungumza Zitto Kabwe mbele ya waandishi wa habari