North Korea wamechukua hatua kali za kulinda siri za nchi baada ya kukerwa na vitendo vinavyo ashiria uvujaji wa siri za nchi hio. Kwa muda sasa North Korea imekua ikijitahidi kupambana na uvujaji wa taarifa kutoka nchini humo kwenda kwenye mtandao wa Instagram ambao baada ya jitihada nyingi lengo lao limetimia.
Hali sasa iko hivi watumiaji wa mtandao ya Instagram kupitia application ya ku-repost picha iitwayo Instagram Photo Sharing App wamezuiliwa kushare post zozote zinazo ashiria uvujaji wa siri kutoka nchini himo, na kwa mtu yoyote atakae jaribu kushare picha yoyote inayoashiria kua picha ya kusambaza siri za ndani za nchi wanakutana na ujumbe unaosema; >>>“Onyo! Huwezi kuonganishwa na Website hii kwa sababu imezuwiwa kutumika na application hii”.
Baadhi ya magazeti nchini humo yamesma kwamba maamuzi haya yametokana na mkasa uliotokea June 11 ambako hoteli maarufu nchini humo yene jina Konyo Hotel ilishika moto na kuungua, na licha ya nchi hio kuiweka ishu hio chini ya kapeti baadhi ya wapiga picha walivujisha picha hizo inje ya nchi na kisha picha hizo zika sambaa kwenye mtandao wa Instagram.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.