Mtu wangu unaikumbuka stori ya Simu mpya za Samsung Galaxy Note 7 zinazotengenezwa na kampuni ya Samsung ya nchini Korea Kusini, zilizoingia sokoni August 19, 2016 na kuleta sintofahamu baada ya kuwepo kwa taarifa za ubovu wa betri za simu hizo uliokuwa unasababisha kulipuka.
Taarifa mpya kutoka kampuni ya Samsung zinasema kuwa imeanza kuzibadilisha simu zilizouzwa kwa wateja waliozinunua kutoka maduka ya nchini Uingereza.
Samsung wamewataka wamiliki wa simu hizo zilizoathirika na ambazo ni nzima, kutoa taarifa kwa wauzaji mapema iwezekanavyo, na tayari maduka mengi yameanza kuwasiliana na wa wateja wa mwanzo kuzinunua ili waweze kubadilishiwa kwa kupewa simu za bure kwa wale walioathirika huku wafanyibiashara wa simu hizo wakipewa mzigo mpya ili kufidia gharama zilizotumika wakati Samsung ikitarajia kuingiza sokoni awamu ya pili ya simu hizo wiki mbili kutoka sasa.
ULIPITWA NA KAULI YA RAIS WA TFF KUHUSU KUSAINI MKATABA WA MILIONI 250 ZA VODACOM PREMIER LEAGUE, ITAZAME HAPA