Bila shaka taarifa hii itakua sio nzuri kwa watu wangu wanaopenda bidhaa za Kampuni kubwa ya kutengeza simu aina ya smartphone ya Samsung. Mtandao wa Reuters umeripoti kuwa Samsung wameamua kusitisha utengezaji wa simu aina ya Galaxy Note 7 ili kuzifanyia ukaguzi zaidi.
Leo October 10, 2016 nimezipata sababu kubwa 2 zilizopelekea Samsung kusitisha utengenezaji wa mzigo mwingine na kuziondoa sokoni kwa muda simu hizo ikiwa ni baada ya kampuni kubwa mbili za nchini Marekani AT & T na ile ya Kijerumani ya T-Mobile kukataa kuendelea kuuza simu za Galaxy Note 7.
Sababu hizo ni pamoja na..
- Kukagua kwa undani matatizo ya Betri za simu hizo ili kubaini ubovu wake.
- Kuimarisha utengezaji wa simu hizo ili kuhakikisha ubora na usalama wake
Kampuni ya Samsung leo Jumatatu October 10, 2010 imetangaza kuzuia usafirishaji wa simu hizo katika maeneo tofauti duniani ili kuzifanyia ukaguzi wa kina. Inaelezwa kua taarifa hii imesababisha kushuka kwa thamani ya hisa za kampuni ya Samsung kwenye soko la dunia kwa zaidi ya asilimia 4.
Ikumbukwe kwamba Kampuni hiyo ya Korea Kusini mwezi September ilizirudisha simu hizo na kuwahakikishia wateja wake kwamba simu zilizorekebishwa ziko salama, pamoja na taarifa hiyo ya Samsung bado kumekuwa na ripoti nyingine tofauti za simu zilizorekebishwa kuendelea kutoa moshi au kulipuka.
ULIPITWA UZINDUZI WA SIMU MPYA YA TECNO PHANTOM 6 ILIYOANZA KUUZWA TANZANIA? TAZAMA HAPA