Serikali kupitia Idara ya Habari Maelezo imetangaza kuwa imepokea rasmi na kuridhia taarifa kutoka uongozi wa Kampuni ya IPP ya kujiwajibisha kwa kuomba radhi kwa Rais JPM na Kagame pamoja na kusitisha uchapishwaji wa gazeti la Nipashe Jumapili kwa miezi mitatu.
Hii ni baada ya Jumapili ya jana January 14, 2018 gazeti hilo kuandika habari yenye kichwa cha habari kisemacho “JPM akerwa wanaomtaka adumu Urais kama Kagame“.
“Kwa makosa haya na hatua zilizochukuliwa haraka na wahusika, tunachukua nafasi hii kuwapongeza Wamiliki na Wahariri wa Nipashe Jumapili na IPP Media kwa wao wenyewe kujitathmini, kujikosoa na kujisahihisha.” – Idara ya Habari Maelezo
IGP SIRRO: Wahalifu wa Kibiti baadhi yao wamekimbilia Msumbiji
Alichosema Waziri Ummy alipotembelea Hospitali ya Rufaa Temeke