Ni Julai 29, 2023 ambapo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo anazungumza na Wananchi kweny Mkutano wa Chama ulioandaliwa Kawe Jijini Dar es Salaam huku akiongozana na viongozi mbalimbali wa Chama hicho.
Hapa nimekusogezea Nukuu za jerry Silaa Mbunge wa Ukonga akizungumzia kuhusu Uwekezaji wa bandari.
“Sisi Chama Cha Mapinduzi tunasema kwamba, maoni bado yanapokelewa. Kila mtanzania anaeamini ana maoni ambayo yataboresha; yanakaribishwa na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu na yote yatafanyika katika kulinda masilahi ya mtanzania.” – Jerry Silaa mbunge wa Ukonga
Mkataba ulifika pale bungeni, tuliujadili na tulifanya kazi kwa kipindi kirefu. Wabunge wakaupitia, tukapokea maoni tukayachakata na kuwasilisha taarifa bungeni; tukauridhia na sasa tunaendelea kuisihi Serikali itekeleze kwa haraka; ili wakaone kwa macho yao wenyewe.” Jerry Silaa mbunge wa Ukonga.