Ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ambapo Mei 9, 2024 amewasilisha Bajeti ya Wizara ya Maji kwa Mwaka 2024/25 Bungeni mkoani Dodoma.
Hizi ni nukuu zake alichozungumza Bungeni wakati akiwasilisha Bajeti hiyo.
“Wizara itaendelea kufanya tathmini na ufuatiliaji wa ubora wa maji katika vyanzo vya maji 2,200, mifumo ya Usambazaji maji 8,245 vijijini na mijini na mifumo 150 ya majitaka. Wizara itaendelea kuziboresha maabara za maji kwa kuzipatia vitendea kazi na kuziwezesha kupata na kudumisha hadhi ya ithibati katika viwango vya kimataifa”- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
“Wizara imepanga kuboresha Utoaji wa huduma ya maji kwa kudhibiti bei za maji, kuondoa migawo ya Maji kuunganishia wateja huduma ya maji kwa wakati na kupunguza malalamiko ya Wananchi yatokanayo na huduma ya maji. katika kufikia azma hiyo, Wizara imepanga kusimamia ufungaji wa dira za maji za malipo kabla (Prepaid Water meters) na kuendelea kuboresha mfumo wa pamoja wa Ankara za Maji (Unified Maji Billing System).Lengo ni ku punguza kuwa go cha maji yanayopotea kutoka Wastani wa Asilimia 35.3 hadi kufikia kiwango kinachokubalika kimataifa cha Asilimia 20”- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
‘Kigamboni kutoka kwenye tanki la Kimbiji unatekelezwa kwa Gharama ya Shilingi bilionuz 8 na hadi mwezi April 2024 utekelezaji umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
‘Wizara kwa kushirikiana na Benki ya kiarabu kwa maendeleo ya Afrika (BADEA) na mfuko wa maendeleo wa Saudia (Saudi Fund for Development-SFD) inatekeleza mradi wa maji Mugango, kiabakari na Butiama kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 30.69 Hadi mwezi April 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 98.7 na umeanza kutoa huduma na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2024.Mradi utawanufaisha zaidi ya Wananchi 100,000 waliopo katika eneo la Mradi’- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso