Ni April 4, 2024 ambapo Klabu ya Young Africans tayari ipo nchini Afrika Kusini kwaajili ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns F.C utakaochezwa siku ya Ijumaa Mnamo April 5, 2024 nchini humo.
Hapa nina nukuu za Kocha wa Yanga Miguel Gamondi akifunguka kuelekea kwenye mchezo huo.
“Siwaandai wachezaji wangu kwa ajili ya historia ya Mamelodi, naandaa timu yangu kutokana na dakika 90 zinazokuja. Tunaamini kazi tuliyofanya kwenye Uwanja wa mazoezi, tuna imani na wachezaji na Mashabiki wetu, haitakuwa rahisi kwetu na kwao pia”
“Tuna Wachezaji wenye uzoefu wenye sifa ya kupambana, msimu uliopita kwenye Fainali ya Kombe la Shirikisho walipoteza nyumbani lakini wote mnajua kilichotokea walipokwenda ugenini, kesho ni mchezo tofauti lakini watapambana tena kwa ajili ya mashabiki wetu“- Miguel Gamondi
“Utakuwa mchezo mgumu lakini ni lazima baada ya dakika 90 kuwe na mshindi mmoja. Mpaka sasa mchezo uko 50/50 bado kila timu ina nafasi hivyo tuko hapa kuhakikisha tunapambana kupata matokeo mazuri”- Miguel Gamondi
“Tunasubiri kuona itakavyokuwa leo kwenye mazoezi ya mwisho, tunaweza kumpata mchezaji katika wale waliokuwa majeruhi. Ni kweli tunaiwaza nusu fainali ya CAF lakini tunajali pia na usalama wa afya za wachezaji wetu pia. Young Africans haichezi mashindano haya peke yake” – Miguel Gamondi
“Mechi yangu ya mwisho hapa Afrika Kusini kwenye Uwanja wa Loftus, nilikuwa Kocha wa Platinum Stars na tuliifunga Mamelodi magoli 2-1. Nina heshima kubwa na Nchi hii, nimeishi vizuri na watu wa hapa Lakini kwa sasa nimerudi na Young Africans SC na tunataka kuwafurahisha watu wa Watanzania” – Miguel Gamondi