Ni Julai 30, 2023 ambapo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo anazungumza na Wananchi kweny Mkutano wa Chama ulioandaliwa Mkoani Mwanza.
Hapa nimekusogezea Nukuu za Mkuu wa Wilaya ya Handeni Alberto Msando akizungumzia kuhusu Uwekezaji wa bandari.
‘Ndugu Katibu Mkuu na Wanachi wa Kanda ya Ziwa Mkataba wowote unaposainiwa lazima uwe umesainiwa kwa jambo mahususi ambalo kila mtu anaweza kulifahamu na mkataba tuliosaini sisi umesema tutashirikiana kwenye mambo yalitajwa kwenye kiambatanishi namba moja, sasa hii ipo kwenye mkataba’- Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Alberto Msando
‘Nimewasikia wanasema mkataba hawana masilaha, Wana CCM tembeeni kifua mbele hawana hoja yoyote ya muhimu Mkataba huu nia ni kuendeleza, kusimamia na kuboresha ndugu Katibu Mkuu tulipoingia kwenye huu mkataba tulikuwa na akili timamu tulijua utekelezaji wake unaweza ukafika mahali ukapelekea kufanya marekebisho ni kitu cha kawaida kabisa katika fani ya Sheria fani ya uwekezaji’- Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Alberto Msando
‘Ndugu Katibu Mkuu kifungu namba 22 kinatoa ruksa kwa pande mbili kuweza kufanya marekebisho, Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa mtu mngwana sana na akasema kama unajiona una mawazo yalete tuyasikie’- Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Alberto Msando