Ni Julai 29, 2023 ambapo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo anazungumza na Wananchi kweny Mkutano wa Chama ulioandaliwa Kawe Jijini Dar es Salaam huku akiongozana na viongozi mbalimbali wa Chama hicho.
Hapa nimekusogezea Nukuu za Mhe Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi akizungumzia kuhusu Uwekezaji wa bandari.
“Mpaka muda huu pale bandarini kuna meli 9 zimepaki zikisubiri kushusha mizigo yao na zimeingia tangu mwezi Juni 16, mwaka 2023 na mpaka wakati huu hazijashusha. Kwa hiyo gharama ya yule mfanyabiashara mwenye mzigo ndani ya meli inazidi kuongezeka. Kila siku ya Mungu gharama yake ni Dola za Marekani 25,000 sawa na Sh Milioni 58 kwa siku,”- Mhe Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi.
“[Bandari ya Dar] kuna tatizo la muda wa kusubiri wa kuingia nangani kushusha mzigo. Kwa sababu ya uchache wa magati, hapa kwetu meli zinasubiri takribani siku tano wakati wenzetu Mombasa wanasubiri siku moja tu na saa 6 tu, huku Durban wakisubiri siku moja na saa 5 pekee ili meli ishushe mzigo,”- Mhe Atupele Mwakibete, Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi.