Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amezindua mpango wa masomo ya elimu ya Msingi na Sekondori kwa njia ya radio ikiwa na lengo la kuendeleza ratiba za masomo kwa watoto ili kudhibiti uzurulaji na tabia hatarishi kwa wanafunzi katika kipindi hiki cha mlipuko wa Virusi vya Corona.
RC Mwanri amezindua mpango huo katika kikao cha Baraza la Madiwani na amewataka Wazazi kutoa ushirikiano kwa watoto wao “Tukikaa hapa tusishangae tukirudi tutakutana na kikosi cha mbumbu na nusu ya watoto wetu wa kike ni wake za watu ukiuliza watakujibu Corona”