Mchezaji nyota wa Real Madrid James Rodriguez amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea kwa mkopo mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich ambako atakuungana kwa mara nyingine na Meneja Carlo Ancelotti.
Rodriguez ambaye alitajwa sana kuwindwa na klabu kadhaa za Ulaya ikiwemo Manchester United ya England atafanya vipimo vya afya na miamba ya soka la Ujerumani kabla ya kukamilisha uhamisho kutua Allianz Arena – katika dili abalo linaweza kufikia hadi paundi 40 milioni.
Bayern Munich pia watakuwa na hiyari ya kumnunua moja kwa moja staa huyo wa Kimataifa wa Colombia mwishoni mwa mkataba wake wa mkopo ambapo itakuwa June 30, 2019. Gharama ya mkopo ni paundi 9m wakati kutakuwa na nyongeza ya paundi 31m juu yake kama watamhitaji moja kwa moja.
Kujiunga kwake na Bayern Munich kutamfanya aungane na Carlo Ancelotti meneja wake wa zamani ambaye alimsajili akitokea Monaco katika dili ambalo Real Madrid waliingia gharama ya paundi 63 milioni baada ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.
Katika msimu mmoja wa kuwa pamoja walishinda UEFA Super Cup na FIFA Club World Cup lakini hata hivyo mwishoni mwa msimu wa 2014-15 alishuhudia Carlo Ancelotti akitimuliwa na Rais wa Real Florentino Perez.
EXCLUSIVE: Staa wa Bundesliga mwenye asili ya Tanzania kwa nini anachezea Denmark na sio Tanzania!!!