Nyaraka zilizovuja za Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) na Shirika la Ujasusi la nchi hiyo (CIA) zinaonyesha kuwa Misri imekuwa ikijiandaa kutuma silaha nchini Russia.
Gazeti la Marekani la Washington Post liliripoti siku ya Jumatatu kwa kunukuu nyaraka za Pentagon na CIA, kwamba taarifa zinazodaiwa kutolewa na Marekani zinaonyesha kuwa mwanzoni mwa mwaka huu Misri ilikuwa na mipango ya kuipatia Russia maroketi elfu arubaini kwa siri.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, imeelezwa katika nyaraka hizo kwamba Rais Abdel Fattah Al-Sisi wa Misri, ameamuru uundaji na usafirishaji wa maroketi hayo ufanyike kimya kimya ili usije ukazusha matatizo na nchi za Magharibi.
Misri ni miongoni mwa washirika wakuu wa Marekani barani Afrika, ambayo kwa miongo kadhaa imepokea zaidi ya dola bilioni moja kila mwaka kama msaada wa masuala ya usalama kutoka kwa Marekani.
Kulingana na ripoti hiyo, nyaraka hizo zimegusia pia mipango ya Misri ya kuipatia Russia risasi za mizinga na baruti.
Katika miezi iliyopita, zilitolewa ripoti zilizoeleza kwamba baadhi ya nchi ziko tayari kuimarisha ushirikiano wao wa kijeshi na Russia…