October 14, 2016 Mtu wangu ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 17 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1999. Ayo TV imefika kwenye nyumba ya kwanza aliyowahi kuimiliki Mwalimu Nyerere mwaka 1959 ambapo aliishi kwa miezi 8 wakati akiwa kwenye haraki za kupigania Uhuru wa nchi yetu.
Nyumba hii aliishi yeye na familia yake akiwa na watoto watano mpaka wakati alipohamia Upanga kwenye nyumba ya Waziri Mkuu na baadaye kuhamia Ikulu ya Dar es salaam akiwa Rais wa kwanza.
Ayo TV imezungumza na msimamizi wa nyumba hiyo ambayo kwasasa inafahamika kama Makumbusho ya Mwalimu Nyerere iliyoko Magomeni Usalama, Jijini Dar salaam.
>>>Mwalimu Nyerere aliishi hapa na familia yake na aliitumia nyumba hii kwenye harakati zake za kudai uhuru kwasababu wakati ule alikuwa amejikita sana kwenye siasa baada ya kustaafu kazi ya ualimu katika shule ya Sekondari Pugu. Aliishi hapa kwa miezi nane tu akachaguliwa kuwa Waziri Mkuu akahamia Upanga Sea View:- Msimamizi
Nimekuwekea hapa full Video ya jinsi nyumba ilivyo.
ULIMISS KUONA MSAADA WA MILIONI 10 ALIZOTOA RC PAUL MAKONDA KWA KIJANA ALIYETOBOLEWA MACHO? TAZAMA HAPA CHINI