Ripota wa nguvu Albert G. Sengo kutoka Mwanza anaripoti Mmisionari Simon Nyirani Mhagama wa Shirika la Mt. Kalorilwanga ambaye anasambaza ujumbe kuhusu hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere kuwa Mtakatifu wa 21 tangu tarehe 20/03/2013.
Picha ya mwisho ya Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere aliyopiga kijijini kwake Butiama kabla ya kwenda kupata matibabu nchini Uingereza ambapo alifia katika Hospitali ya Mt. Thomas.
Wakati yote haya yakifanyika kutoka nchini Uganda: Rais Yoweri Museveni, amesema kiongozi bora ni yule anayefuata maagizo ya Mungu na kuwatumikia binadamu wote kwa usawa na haki.
Rais Museveni aliyasema hayo Tarehe moja mwezi June, wakati wa ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenyeheri na hatimaye kutangazwa mtakatifu.
Picha ya mchoro wa Mtakatifu Charles Lwanga aliyemtangaza Hayati Baba wa Taifa kuwa Mtakatifu wa 21 ambapo alisema hata kwenye maandiko matakatifu ya Biblia kuna mistari inayomtaka binadamu ampende binadamu mwenzake kama anavyojipenda yeye.
Rais Museveni alisema anatarajia kupeleka ushahidi kwa Papa Benedict kwamba Mwalimu Nyerere ana sifa za kutangazwa kuwa mtakatifu kwa sababu alimtii Mungu na kuwatumikia binadamu.
Mmisionari Simon Nyirani Mhagama wa Shirika la Mt. Kalorilwanga ambaye anasambaza ujumbe kuhusu Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere kuwa Mtakatifu wa 21 akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliotembelea kaburi la Baba wa Taifa Butiama mkoani Mara.
Kufuatia hatua hiyo ya kwenda Roma kutoa ushahidi, Rais Museveni amesema katika maadhimisho ya kuombea mchakato wa Mwalimu kuwa Mtakatifu yatakayofanyika mwakani, ameahidi kuwaita maraisi wote waliowahi kufanya kazi na Mwalimu Nyerere ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa Marehemu Baba wa Taifa ameweza kuwa unganisha Waafrika.
Alifafanua kuwa Mwalimu ametoa mchango mkubwa wa ukombozi kwa nchi za Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika Kusini, Uganda na Tanzania yenyewe. Hivyo kuja kwa viongozi hao kushiriki ibada hii itakuwa Baraka kubwa.
Kwa kanisa katoliki utakatifu ni hatua ya tatu baada ya hatua ya kwanza ambayo ni Mtumishi wa Mungu,hatua ya pili ni Mwenye Heri na hatua ya tatu ni Mtakatifu ambapo miujiza mbalimbali pamoja na taarifa hukusanywa kupelekwa makao makuu ya Kanisa hilo.
Ungependa stori kama hizi zisikupite? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.