Mdahalo wa kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere kujadili mfumo wa demokrasia ya vyama vingi umefanyika leo Septemba 20, 2022
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Taasisi ya The Mwalimu Nyerere, Prof. Francis Matambalya, amesema kuwa mdahalo huu u
“Tutajadili mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, wanaionaje. Wajibu wa viongozi wa vyama vya siasa, nafasi kurasimisha mfumo wa vyama vingi, uhusiano kati ya dola na vyama vya siasa, sera, Katiba, sheria, kanuni na taratibu,” amesema Prof.Matambalya
“Kutakuwa na wawakilishi wa makundi mbalimbali yakiwemo ya wanasiasa, Bunge, Serikali na asasi za kiraia zinazosimamia makundi ya watu wenye ulemavu. Tutabadilisha mawazo na kujifunza kuhusu midahalo kama hii tulioifanya Zanzibar na Tanzania bara”-
“Tutazungumzia sababu na historia ya kufanya mdahalo na tulichojifunza kwa wenzetu wa Zanzibar na Tanzania bara. Mwisho wa siku tutakuwa na majumuisho ya masuala mahsusi yatakayopewa uzito katika mdahalo huu utakaowashirikisha wageni kutoka Kenya na Uganda,” amesema Profesa Matambalya.
Kwa mujibu wa Profesa Matambalya, miongoni mwa mambo yaliyobainika katika midahalo iliyofanyika Tanzania bara na Zanzibar kwa nyakati tofauti ni mpasuko kati ya wanasiasa na vyama vya siasa nchini.
Alisema suala ni miongoni mwa mambo yaliyojitokeza katika kuishi demokrasia ya vyama vingi.