Tukio la kuungua moto nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu lilotokea usiku wa Novemba 14, 2020, linaeendelea kuchunguzwa na kamati maalumu ambayo iliundwa na Mkuu wa Mkoa.
Akiongea leo Desemba 8, mbele ya kikao cha kwanza cha Madiwani ambacho kilikuwa maalumu kwa ajili ya kuwaapisha, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Fabian Manoza amesema kuwa uchunguzi wa kamati hiyo bado unaendelea.
Manoza ametoa maelezo hayo, baada ya Madiwani wa Halmashauri hiyo, kutaka kupewa majibu ya nini chanzo cha tukio hilo pamoja na mali ambazo ziliharibika, ambapo majibu yote yatatolewa na tume hiyo mara baada ya uchunguzi kukamilika.
MAALIM SEIF AFUNGUKA YA MOYONI “UCHAGUZI UMETUACHA NA MAAFA MAKUBWA, HAYA NI MAMBO YA AIBU”