Club za Tanzania zinaendelea kuandamwa na jinamizi baya katika michuano ya SportPesa Cup inayoendelea kwa sasa jijini Dar es Salaam, kabla ya hapo vilabu shiriki vya Tanzania vimekuwa na wakati mgumu kutwa Kombe hilo hususani timu za Simba na Yanga zinazoaminika kuwa ni kubwa nchini na kuwa na uwezo wa kupambana.
Simba SC ambao msimu uliopita walipoteza katika fainali ya michuano hiyo dhidi ya Gor Mahia, safari hii imeshindikana kurudia rekodi yao na wamejikuta wakitolewa katika hatua ya nusu fainali kwa kufungwa kwa magoli 2-1 dhidi ya club ya Bandari FC ya Kenya.
Kwa maana hiyo Simba sasa wanasubiri kucheza game ya kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya timu itakayopoteza katika game ya nusu fainali ya pili inayozikutanisha timu za Mbao FC dhidi ya Kariobangi, mshindi wa Kombe la SportPesa safari hii licha ya kutwaa taji hilo atapata nafasi ya kucheza game ya kirafiki dhidi ya Everton katika ardhi ya taifa lake.
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”