Bado Old Trafford kuna fuka moshi kutokana na mahusiano ya kocha wa Man United Jose Mourinho na mchezaji wake Paul Pogba kudaiwa kuweka makundi mawili kutokana na wawili hao kila mmoja kuwa na watu wanaomuunga mkono.
Mourinho kwa sasa anadaiwa kuwa amebakiza saa 24 ndani ya club ya Man United na endapo atapoteza mchezo wa EPL dhidi ya Newcastle weekend hii, inasemekana kuna uwezekano mkubwa wa Mourinho kupoteza kibarua chake.
Leo kilichoripotiwa ni kuwa Mourinho amepoteza ushirikiano kutoka chumba cha kubadilishia nguo cha Man United, wengi wao wanadaiwa kuwa upande wa Pogba, sababu kubwa inayodaiwa kutoka ndani ya chumba cha kubadilishia nguo inaeleza hawakubaliani nae.
Kwa mujibu wa Mirror Mourinho anadaiwa kutokuwa katika maelewano mazuri na Pogba, Sanchez na nahodha wa Man United Valencia kwa madai ya kuwa Mourinho ana maneno ya kukwaza sana na yanavunja moyo na hali ya kujiamini kwa wachezaji wake.
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga