Katika taarifa nadra kutoka kwa Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama alionya kwamba “mkakati wowote wa kijeshi wa Israel ambao hauzingatii gharama za kibinadamu unaweza kurudisha nyuma.”
“Tayari, maelfu ya Wapalestina wameuawa katika shambulio la bomu huko Gaza, wengi wao wakiwa watoto. Mamia kwa maelfu wamelazimika kutoka makwao,” Obama alisema katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii.
Pia alikosoa uamuzi wa serikali ya Israel kukata chakula, maji na umeme hadi Gaza akisema “kwa raia waliotekwa unatishia sio tu kuzidisha mzozo wa kibinadamu unaoongezeka.”
“Inaweza kuzidisha misimamo ya Wapalestina kwa vizazi vingi, kuondosha uungaji mkono wa kimataifa kwa Israel, kucheza mikononi mwa maadui wa Israel, na kudhoofisha juhudi za muda mrefu za kufikia amani na utulivu katika eneo hilo,” alisema rais huyo wa zamani wa Marekani.