Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema usambazaji wa misaada ya kibinadamu katika maeneo mengi nchini Sudan umekumbwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kukosekana kwa usalama na ukosefu wa pesa taslimu, uporaji, urasimu, mawasiliano duni ya mtandao na simu na ukosefu wa wafanyakazi wa kibinadamu na kiufundi.
Pia OCHA imeongeza kuwa ukosefu wa nishati pia umeleta taabu kwa kazi hiyo ya usambazaji pamoja na uzalishaji wa umeme kwa ajili ya uhifadhi wa mnyororo baridi na usambazaji wa maji.
Licha ya hayo OCHA imesema hadi kufikia Januari 4 mwaka huu, mpango wa misaada ya kibinadamu wa 2023 kwa Sudan uliorekebishwa ulifadhiliwa kwa asilimia 40.8 tu.
Nchini Sudan, karibu watu milioni 25 watahitaji usaidizi wa kibinadamu mwaka 2024, lakini ukweli mbaya ni kwamba kuongezeka kwa uhasama kuna waweka wengi wao nje ya uwezo wa kupatiwa usaidizi wa kibinadamu amesema mkuu huyo wa OCHA.
“Usafirishaji katika mstari wa mapigano umesimama, ingawa operesheni ya misaada kutoka Chad kupitia mpaka inaendelea kuwa mkombozi kwa watu Darfur, juhudi za kusambaza misaada mahali pengine zinazidi kuwa hatarini”.