Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa mara nyingine, imevunja rekodi kwa kukusanya jumla ya kiasi cha sh. trilioni 1.987 kwa mwezi December 2019 ambayo ni rekodi ya kwanza kufikiwa tangu kuanzishwa kwake ikilinganishwa na rekodi ya mwezi Septemba, 2019 iliyokuwa sh. trilioni 1.767.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM, Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Edwin Mhede amesema kuwa, makusanyo hayo ya mwezi Desemba 2019 ni sawa na ufanisi wa asilimia 100.20 kutoka katika lengo la kukusanya kiasi cha sh. trilioni 1.983 kwa mwezi huo.
“Ni kweli kwamba, kitaalam, miezi tofauti hailinganishiki moja kwa moja. Hata hivyo, kwa makusanyo haya ya sh. trilioni 1.987 kwa mwezi Desemba 2019″ Mhede
“TRA imevunja rekodi yake yenyewe iliyoiandika mwezi Septemba 2019 ambapo ilikusanya jumla ya sh. trilioni 1.767 ikiwa ni sawa na asilimia 97.20 ya lengo la kukusanya sh. trilioni 1.817 katika kipindi hicho” Mhede.
“Makusanyo haya ya robo ya pili ya mwaka 2019/20 ni sawa na ukuaji wa asilimia 19.78 ikilinganishwa na kipindi kama hiki cha Robo ya Pili ya mwaka 2018/19 ambapo Mamlaka ilikusanya sh. trilioni 4.151 ikiwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 87.59 kutokana na lengo la kukusanya mapato kiasi cha sh. trilioni 4.739 katika kipindi hicho,” Mhede