Kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliambia AFP Jumatano kwamba hatafanya mazungumzo na Rais William Ruto bila mpatanishi wa chama cha tatu baada ya miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya serikali.
Msimamo huu wa Odinga unakuja baada ya Ruto kusema kuwa, yupo tayari kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na mpinzani wake baada ya kushuhudiwa maandamano ya wiki kadhaa, kupinga kupanda kwa gharama ya maisha, miongoni mwa mambo mengine, yaliyosababisha maafa na majeruhi ya waandamanaji.

Tangu Odinga awasihi Wakenya kujitokeza barabarani mwezi Machi, muungano wake wa Azimio umefanya maandamano ya siku tisa dhidi ya serikali, huku maandamano hayo wakati mwingine yakizidi kuwa uporaji na kusababisha vifo kutokana na mapigano na polisi.