Watu wasiojulikana wamevunja Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jimbo la Mbeya Mjini na kuteketeza kwa moto baadhi ya nyaraka muhimu za chama hicho zikiwemo fomu za wagombea ubunge wa viti maalumu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, John Mwambigija, ameliomba Jeshi la Polisi Mkoani humo kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kuwabaini waliohusika na tukio hilo huku akiwataka wanachama wa chama hicho kutolipa kisasi hata kama wanamfahamu aliyetekeleza uhuni huo.