Jumamosi ya June 30 2018 hatua ya 16 bora ya michuano ya World Cup 2018 ilianza rasmi ikiwa ni siku moja imepita toka hatua ya makundi imalizike, mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ulikuwa ni mchezo kati ya Ufaransa dhidi ya Argentina.
Ufaransa wameendeleza rekodi yao kama ilivyokuwa katika hatua ya makundi kwa kuiadhibu Argentina kwa magoli 4-3, licha ya kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa lakini kucheza kitimu zaidi kuliinusuru Ufaransa kwani baada ya kufunga goli la kwanza kwa penati dakika ya 13 kupitia Griezmann.
Argentina wakasawazisha dakika ya 41 kupitia kwa Di Maria na dakika ya 48 wakaongeza goli la pili kupitia kwa Mercado, Ufaransa waliendelea kuwa na utulivu zaidi na na kupata goli matatu ndani ya dakika 11 dakika ya 57 Pavard akafunga goli la kusawazisha na baadae Kylian Mbappe dakika ya 64 na 68 akafunga goli la tatu na nne.
Pamoja na kuwa Argentina walizidisha makali na kuhakikisha wanasawazisha jitihada zao ziliwasaidia kupata goli la tatu dakika ya 93, kipigo hicho kinawaoondoa rasmi Argentina, hivyo sasa Ufaransa anasubiri mshindi wa game kati ya Uruguay na Ureno ndio atakutana nae robo fainali.
Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake