Baada ya kukaa mwezi mmoja na siku 22 rumande kijana Daniel Jones mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni raia wa Uingereza amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kukutwa na hatia ya kuandaa party na kuitangaza kwa kutumia picha za ponografia.
Kijana huyo ni miongoni mwa wenzake 10 ambao walikuwa ni wageni nchini humo ambao pia walihudhuria sherehe hiyo huko Cambodia mnamo January 25, 2018.
Jaji Um Chan Thol ambaye ndiye aliyetoa kifungo hicho ameeleza kuwa kijana huyo Daniel aliweka picha hizo kutangaza party hiyo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, jambo ambalo limevunja kanuni na maadili ya utamaduni wa Cambodia.
Mchungaji awalazimisha Waumini kubusu na kulamba viatu vyake