Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu kwa fainali ya EFL Cup kati ya Chelsea dhidi ya Man City kujua timu gani itakuwa Bingwa, mchezo huo ulimalizika kwa rekodi nyinginge kuvunjwa baada ya Chelsea iliyo chini ya kocha Maurizio Sarri na Man City iliyo chini ya kocha Pep Guardiola kushindwa kupata mshindi kwa dakika 90.
Game haikuwa rahisi kama wengi walivyodhania na hatimae kulazimika kwenda dakika 120 ila mambo yakawa magumu kwa pande zote mbili, ndipo mikwaju ya penati ilipoamua timu gani iwe Bingwa, Chelsea licha ya kuwa imara na kudhibiti mashambulizi ya Man City lakini walijikuta wakipoteza kwa penati 4-3.
Hii ndio mara ya kwanza kwa mchezo wa fainali ya EFL Cup kuchezwa dakika 120 pasipo kupatikana Bingwa toka mwaka 2016, ambapo Man City aliibuka tena Bingwa wa michuano hiyo, Man City sasa wanazidi kumuweka kocha Maurizio Sarri katika wakati mgumu na kibarua chake baada ya kipigo hicho.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake