Baada ya headline mbalimbali zilizokuwa zikimhusisha Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga Emmanuel Okwi hatimae amezungumza kuhusu taarifa hizo ambapo amesema hataki kuzisikia wala kuzungumzia habari za Simba na Etoile du Sahel kwa kuwa hana mpango wa kurejea alikotoka.
Emanuel Okwi ametoa tamko hilo ikiwa ni siku chache mara baada ya kusimamishwa kwa muda,huku uongozi wa Yanga ukisisitiza kuwa utamtumia mchezaji huyo katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine ya Comoro inayotarajiwa kuchezwa wiki ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Okwi ambaye ni raia wa Uganda amesema yeye ni mchezaji wa Yanga na mapenzi yake yapo klabu hiyo ndiyo maana hataki kuzungumzia suala la mgogoro wa usajili wake, kwa kuwa hana mpango wa kurudi alipotoka.
Okwi alianza kwa kusema>>’Najua baada ya muda TFF itaniruhusu kucheza,sitaki kurudi nilipotoka kwa kulizungumzia suala la Etoile (du Sahel), pia sitaki kuizungumzia Simba kwa kuwa siyo klabu yangu’
‘Naipenda Yanga na mapenzi yangu yote yapo hapa, ndiyo maana leo hii nipo klabuni nikiwa mchezaji wao. Nilikuwa tayari kuanza kuichezea Yanga katika ligi hii (mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara) na Ligi ya Mabingwa Afrika’.
Kuhusu suala la sakata la kuzuiliwa kucheza Okwi,Katibu Mkuu wa Yanga Beno Njovu amesema kuwa watamtumia Okwi katika mechi dhidi ya Komorozine kwa kuwa wamepata ruhusa ya kumtumia kutoka Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).
Source:Salehjembe