Mwanamziki mkongwe wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi ambaye aliyetunukiwa tuzo ya tatu iliyobeba heshima ya udaktari kutokana na kuwa mshauri na balozi mzuri wa muziki.
Mwaka 2003 alitunukiwa tuzo kubwa ya heshima na chuo kikuu cha Zimbabwe kwa kutambua miongo kadhaa ya mchango wake na kujitolea katika kujenga muziki na msukumo wa wasanii wa kizazi kipya nchini Zimbabwe huku akionyesha ushawishi kwenye kazi za wasanii hao.
Oliver Mtukudzi anatarajiwa kutoa burudani kwenye tamasha la Vibe East Africa litakalofanyika leo August 6 2016 kwenye ukumbi wa nafasi Art jijini Dar es salaam, akiwa na wengine ambao ni Eric Wanainai kutoka Kenya, Jemima Sanyu, Slim MC ‘Uganda’.
Akizungumza jijini Dar es salaam Oliver Mtukudzi ametoa amezungumzia siri ya aina ya muziki wake wa ‘Tuku Music’ kufanikiwa kimataifa na ameutoa ushauri huu kwa wasanii wa bongo………
>>>’mimi ni mimi, na ninafanya mimi kama mimi siwezi kuwa na mshindani hata kidogo niko kama kamungu kadogo duniani kote, kwahiyo nawaomba wasanii wa Tanzania wafanye kama watanzania, waoneshe kwamba wao ni watanzania na hawatakuwa na washindani hata kidogo na watu wataupenda na kuutaka muziki wao duniani kote’
ULIKOSA HII YA DIAMOND KWENYE SHOW YA ONE AFRICCA MUSIC FESTIVAL NEW YORK MAREKANI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI