Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Ole Nasha bado anaendelea na ziara yake Kanda ya Ziwa akikagua utekelezaji wa Miradi ya elimu inayotekelezwa na Wizara kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R – Education Perfomance for Result).
Leo March 5, 2018 yuko mkoa wa Shinyanga ambapo ametembelea shule ya Msingi Buhangija ambayo nayo inatekeleza programu ya Lipa Kulingana na Matokeo na imepatiwa fedha kiasi cha Milioni 286,600,000 kwa ajili ya kujenga madarasa, mabweni mawili na vyoo.
“Bweni linagharimu kiasi cha Milioni 75 na linatakiwa kuchukua wanafunzi 80, sasa shule hii wametumia Milioni 75 kwa kila bweni kujenga lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 48 kinyume na maelekezo ya serikali kuwa wanapaswa kujenga mabweni yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 80 kila moja kwa Milioni 75,” -Ole Nasha
KATIBU MKUU CHADEMA NA VIONGOZI WENGINE BAADA YA KUTOKA POLISI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
MAHAKAMA YA RUFAA DHAMANA YA RUGEMARILA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA