Leo February 11,2020 Baraza la mpito nchini Sudan limekubali kumkabidhi Rais wa zamani Omar al Bashir kwa Mahakama ya kimataifa ya ICC.
Omar al Bashir alikuwa akitafutwa kutokana na makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu.
Mwezi December Kiongozi huyo wa zamani aliyeondolewa madarakani kwa mapinduzi mwezi Aprili, alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na kituo cha marekebisho ya tabia kwa makosa ya rushwa.