Mchekeshaji maarufu nchini Kenya aliyegeukia harakati za kisiasa Eric Omondi ametangaza kuanzisha mchakato wa kura ya maoni ya kupunguza kaunti (kanda/majimbo) ya nchi hiyo kutoka kaunti (47) zilizopo sasa hadi kaunti nane (8).
Omondi anadai kuwa wingi wa kaunti hizo unachangia kuongezeka kwa mianya ya rushwa, ufinyu wa huduma kwa umma na kuongeza mzigo kwa wananchi walipa kodi wa nchi hiyo.
Ameandika “tumezindua rasmi mchakato wa kwenda kwenye kura ya maoni ya kupunguza idadi ya kaunti kutoka 47 hadi 8, tunakwenda kukusanya maoni sahihi ili kuanza mchakato huo.
Wakenya WANAWAKILISHWA SANA NA VIONGOZI WENGI SANA, nia ilikuwa kusambaza huduma lakini tukaishia kusambaza rushwa, MLIPA KODI AMEZIDIWA MZIGO.”
Wingi wa kaunti nchini humo umefanya wawakilishi wa wananchi kuwa wengi maradufu, mtu mmoja akiwakilishwa na viongozi takribani 16, mchekeshaji huyo amesema katika tangazo hilo.