Najua kuna list kubwa ya watu wa nguvu ambao walikuwa na hamu kuishuhudia stage ya burudani ya nguvu ya FIESTA ambayo huwa inatolewa kila mwaka kwenye mikoa mbalimbali ya TZ… 2015 mzigo upo?!
Boss wa Clouds FM, Ruge Mutahaba ana majibu kuhusu uhakika wa FIESTA mwaka 2015 ambapo amesema kwa sababu ya shughuli za Uchaguzi Mkuu imebidi FIESTA isiwepo ili kutoa muda wa maandalizi mazuri na ya nguvu zaidi kwa ajili ya mzigo mzima wa FIESTA 2016 !!
List ya mastaa wa muziki waliomaliza elimu za juu vyuoni imezidi kupanda ambapo kwenye waliomaliza Vyuo 2015 wakali toka Dodoma, Slim Sal pamoja na Moni nao wamo.
Mbunge wa Dodoma kaamua akutane na wakali hao wa muziki kutoka Dodoma ambao wamefanikiwa kumaliza elimu za juu Vyuoni na kuona jinsi ya kuwasaidia ili kuupa support muziki wa vijana hao.
Tattoo za Q Chief unazijua zote? Basi sikia hii mtu wangu, jamaa amesema anazo kama 40 hivi ila kuna nyingine ziko sehemu za siri ambazo mtu mwingine hawezi kuziona… Kingine amesema kwenye hizo zote tattoo 40 hakuna ya mwanamke hata mmoja kwa sababu anahisi kama mambo yakienda vibaya baadae uhusiano ukayumba, itamuweka kwenye wakati mgumu.
Story zote hizi hapa kwenye audio kabisa mtu wangu
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE