Katika kuhakikisha ajali za moto Shuleni zinadhibitiwa, Serikali imesema hakuna Shule itakayoruhusiwa kufanya shughuli zake bila kuwa na vifaa muhimu vya kujikinga dhidi ya majanga ya moto.
Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Joseph Mwasabe ameonya Shule zitakazoshindwa kufanya hivyo zitafutiwa leseni na zile zenye uhaba zitapewa muda kujirekebisha kabla hatua stahiki hazijachukuliwa.
Katika kuhakikisha Wanafunzi wanalindwa, amesema wamefanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini endapo Shule zinazingatia Sheria zilizowekwa.