Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA, imetoa tahadhari ya uwepo wa Mvua kubwa, kuanzia Disemba 21 hadi 22, 2019, kwa Mikoa ya Dar es Salaam, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma, Visiwa vya Unguja na Pemba, Zanzibar, Pwani, pamoja na Mikoa ya Morogoro, Singida, Dodoma, Lindi,Mtwara,Rukwa na Mbeya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, imeeleza kuwa upo uwezekano pia wa mvua hiyo kuendelea na siku ya kesho ya Disemba 22, 2019, kwa baadhi ya mikoa ikiwemo ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma, Singida, Dodoma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Athari ambazo zimeelezwa kujitokeza ni pamoja na uharibifu wa miundombinu na mali kwa baadhi ya miundombinu maeneo.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa upo uwezekano wa Mvua hizo kuendelea kunyesha, hadi siku ya Jumanne ya Disemba 24 kwa baadhi ya Mikoa ya Njombe, Iringa, Rukwa, Ruvuma, Songwe na maeneo ya Kusini mwa Mkoa wa Morogoro.
MEYA AOMBA ULINZI AKIOGOPA WATOTO WA IBILISI, WANAOPORA NA KUPIGA