Leo March 14, 2018 Mtandao wa wanafunzi nchini Tanzania (TSNP) umesema taarifa za nini kilichomkuta Abdul Nondo zinakinzana.
“Sisi bado hatuamini Uchunguzi uliofanywa na polisi kwa kuwa hatujamsikia Nondo akiongea na kile tulichoelezwa na polisi mkoani Iringa na hiki tulichokisikia leo kwa polisi Dar es Salaam haviendani”, -Msemaji wa TSNP Helllen Sisya aliiambia BBC.
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania ambao ulitoa taarifa kwa Umma kuhusu kupotea kwa Abdul Nondo, hawakubaliani na taarifa hiyo ya polisi kwa kudai kuwa inakanganya, Polisi wanadai kuwa alipatikana akiendelea na shughuli zake za kawaida alipoenda kumtembelea mpenzi wake na wakati wao walipata taarifa kutoka kwa jeshi la polisi wa Iringa kuwa Nondo alifika kituoni hapo akiwa hajitambui.
BREAKING: ‘NONDO ALIKWENDA KWA MPENZI WAKE” -POLISI DSM