Katika dakika chache zilizopita, msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) Admiral Daniel Hagari amekuwa akitoa taarifa kuhusu mzozo huo.
Tayari tumesikia kutoka kwa IDF asubuhi ya leo, wakidai kuwa wameua “dazeni” za wanamgambo wa Hamas usiku kucha.
Bw Hagari anasema vikosi “vinaendelea hatua kwa hatua” huko Gaza kama sehemu ya operesheni ya ardhini na kumekuwa na “mawasiliano ya moja kwa moja” na wapiganaji wa Hamas.
Pia anaonya kwamba shughuli “zitaongezeka” na askari wamewekwa “tahadhari kubwa” kwenye mpaka wa kaskazini.
“Shughuli zetu na operesheni zitaendelea na kuongezeka kulingana na hatua za vita,” anaongeza.
“Hii ni operesheni iliyopanuliwa ya ardhini kwenye ukanda huo. Vikosi vya ardhini, vifaru, vikosi vya askari wa miguu, vikosi vya jeshi vinaelekea kwa magaidi,” alisema.
“Magaidi hao walijikusanya katika maeneo fulani ili kujaribu kulenga vikosi vyetu na tunavishambulia kutoka angani, ndivyo tulivyoweza kuwashambulia na kuwalenga magaidi 20.
“Pia kuna mawasiliano ya moja kwa moja kati ya vikosi vya ardhini na magaidi. Mapigano yanaendelea ndani ya Ukanda wa Gaza.”