Watanzania wana kila sababu ya kufurahi kwa kuwa sasa watakuwa na nafasi bora zaidi za kuchagua vifaa bora vya mawasiliano baada ya kampuni ya simu ya OPPO kuzinduliwa rasmi nchini Tanzania
Akizungumza jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne wakati wa uzinduzi wa bidhaa hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa OPPO Tanzania, Kenny Yue alitangaza rasmi kuingizwa katika soko laTanzania bidhaa zake nchini Tanzania zijulikanazo ka ‘OPPO A series’.
Bw Yue alisema kuwa kwa kawaida mtumiaji wa simu anaangalia vipengele muhimu wakati wa kubadilisha simu za mkononi, ikiwemo matatizo ya kiufundi, bei, huduma za kibunifu, chapa, umahiri na sifa nyingine nyingi za kimsingi, ndio maana OPPO imeshughulikia vipengele hivi vyote.
Alisema OPPO ilianzishwa mwaka wa 2008, na hadi sasa imejiweka vizuri kutoa teknolojia iliyo bora kwa watumiaji wake, na kuongeza kuwa kwa sasa kampuni hiyo inajivunia kuwahudumia watumiaji katika nchi zaidi ya 60 ulimwenguni.
“Tangu kuingia kwetu kwa mara ya kwanza katika bara hili la Afrika, OPPO imekuwa na mafanikio katika masoko mbalimbali katika nchi kama vile Misri, Morocco, Kenya na Afrika Kusini, na kuingia kwetu Tanzania ni uthibitisho wa dhamira yetu isiyoyumba ya kuifanya dunia kuwa mahali pa furaha kupitia teknolojia bora kwa watumiaji wetu wote, “alisema.
Alisema kuwa ripoti za hivi karibuni kutoka Canalys zimeonyesha hisa ya soko ya OPPO imekua kwa asilimia 73 kila mwaka, ikishika nafasi ya 4 katika bara la Afrika.
“Hii inaonyesha kuwa uwekezaji wetu katika masoko mapya kama vile Tanzania unaendelea kuonyesha imani na kujitolea kwetu kwa watumiaji wetu,” aliongeza.
Kuhusu bidhaa mpya katika soko la Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema mbali ya bidhaa zao za aina ya A Series, OPPO Tanzania inakusudia kutambulisha bidhaa zake za hadhi ya juu sokoni hivi karibuni, kama vile mfululizo wa Reno10 na Find N series.
“Tunapoanza safari hii ya kusisimua, tunawahakikishia wateja wetu kuleta teknolojia bora na bidhaa katika soko hili,” Farida Mwangosi, Meneja wa Bidhaa wa OPPO alisema.
Alisema kuwa OPPO inapeperusha bendera yao katika zaidi ya nchi 60, ikiwa na zaidi ya wafanyikazi 40,000 waliojitolea kuhakikisha wateja wao wanapata bidhaa na huduma bora.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na msanii maarufu wa Muziki wa Bongo Flava Jux ambaye ni mmoja wa wahamasishaji wakubwa wa bidhaa za OPPO pamoja ya Rommy James, Official 9 na DJ Muumy.