Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Brazil sasa imefikia zaidi ya Milioni Mbili, huku idadi ya vifo ikiongezeka pia na kufikia zaidi ya 76,000.
Wizara ya Afya nchini humo imesema Watu wengine zaidi ya 45,000 walipatikana na janga hilo kwa muda wa saa 24 zilizopita, huku wengine 1,300 wakipoteza maisha.
Ongezeko hili linaifanya Brazil kuwa nchi ya pili duniani kuumizwa zaidi na virusi hivyo baada ya Marekani ambayo ina Wagonjwa milioni tatu na laki tano hadi sasa ambapo kwa kipindi cha miezi miwili taifa hilo la Amerika Kusini limekuwa likiripoti maambukizi mapya zaidi ya elfu 30 kila siku na mara 11 imeripoti Wagonjwa zaidi ya elfu 40.
Watalaam wa afya nchini humo wamemlaumu Rais Jair Bolsonaro ambaye pia ameambukizwa virusi vya corona kwa kushindwa kuja na mpango wa kudhibiti maambukizi hayo.