Mwanariadha maarufu kutoka South Africa Oscar Pistorius, aliingia kwenye headlines baada ya kesi ya yeye kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp siku ya wapendanao mwaka 2013 kushika uzito mkubwa nchini South Africa… kesi ikaenda Mahakamani na Oscar akasema hakudhamiria kufanya vile, ilikuwa ni bahati mbaya kwani aliamini kuwa waliingiliwa na mwizi nyumbani kwao… mwisho wa siku Mahakama ikaamua kumpatia Oscar adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela!
Mwaka jana Mahakama ilisema kuwa kitendo alichokifanya Oscar Pistorius kilikuwa ni “uzembe” lakini hakiashirii mauaji wala hakikuonyesha dhamira ya kuchukua maisha ya mpenzi wake… Hiyo ilikuwa ni October mwaka 2014 na kipindi chote hicho Oscar alikuwa jela.
Headlines zilibadilika siku ya jumatatu baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Oscar Pistorius atatolewa jela na kuwekwa chini ya ulinzi kwa kutumikia kifungo cha nyumbani baada ya Bodi ya Parole nchini South Africa kupitisha kifungo hicho kwa miaka minne.
Leo vyombo vya habari vimeripoti kuwa Oscar ametolewa jela na ataanza kutumikia kifungo chake cha nyumbani kwa mjomba wake jijini Pretoria, South Africa na Sheria za South Africa hazimruhusu Oscar Pistorius kufanya chochote mpaka kifungo chake kitakapoisha ila atatakiwa kufanya kazi za kijamii ikiwa ni sehemu ya vigezo alivyowekewa na Bodi ya Parole ya South Africa.
Wanasheria wa Serikali wameanza maandalizi ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ya Mahakama kwa kuamini kuwa Oscar Pistorius ambaye ana miaka 28 sasa, anatakiwa ahukumiwe kwa kosa la mauaji… Rufaa hiyo inategemewa kusikilizwa mwezi ujao.
Unaweza pia ukatazama video hii hapa chini kwa taarifa zaidi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE