Habari ya Asubuhi..!Karibu kwenye matangazo yetu hii leo Jumatano,9.8.2023
Kiongozi wa upinzani nchini Senegal ambaye amekuwa kwenye mgomo wa kula akipinga kuzuiliwa kwake
Ousmane Sonko alilazwa Jumapili katika Hospitali Kuu katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, kulingana na taarifa kutoka kwa chama chake kilichovunjwa sasa, Patriots of Senegal (PASTEF).
Sonko, 49, alikamatwa mnamo Julai 28, na ameshtakiwa kwa kupanga uasi, kudhoofisha usalama wa serikali na ushirika wa uhalifu na kundi la kigaidi.
Sonko alitangaza mnamo Julai 30 kwenye jukwaa X, ambalo zamani lilijulikana kama Twitter, kwamba angeanza mgomo wake wa kula.
Tangazo hilo lilikuja siku moja kabla ya jaji katika mji mkuu wa Dakar kuamuru kufungwa kwake.