Leo July 2, 2018 Rais Dkt. John Magufuli amezindua kitabu cha Dkt. Reginald Abraham Mengi kilichopewa jina la ‘I Can, I Must, I Will- The Spirit of Success’ katika hoteli ya Serena Jijini DSM.
Nakusogezea NUKUU 7 kutoka kwa Rais Magufuli ambapo amemchangia Milioni 10 Msichana Wakonta Kapunda kutoka Tanzania anayeandika kwa kutumia ulimi wake. Ambaye pia ni miongoni mwa washindi washindano la kuandika wazo la Biashara lililoandaliwa na Dr. Reginard Mengi.
Rais Magufuli ametoa wito “Kitabu cha Mzee Mengi kiwe fundisho kwetu sote, nitoe wito kwa wafanyabiashara wote msisikilize maneno ya watu wanaowakatisha tamaa, fanyeni biashara kweli kweli”
Jambo la tatu ni kuhusu mtazamo wake kabla hajawa Rais “Nilijua ukishakuwa Rais huwezi kukatishwa tamaa na mtu yeyote kwa sababu wewe ni Rais lakini haikuwa hivyo, nilipoingia niliyaona” – Rais Magufuli
Nukuu ya nne ni “Nina matumaini makubwa kupitia kitabu chako hiki watanzania wengi watajenga matumaini, kujiamini na mafanikio makubwa na katika hili naomba kitabu hiki ukitafasiri kwa lugha ya kiswahili ili kupata fursa ya watanzania wengi kukisoma” – Rais Magufuli
JPM ametoa wito kwa watanzania “Watanzania tuache kukatishana tamaa na ninafahamu katika historia ya Mzee Mengi yapo mengi amepambana nayo ya kukatishwa tamaa” – Rais Magufuli
Rais amezungumzia alichojifunza “Funzo la kwanza nililopata kutoka kwenye kitabu hichi alichokiandika Mzee Mengi kuwa sisi Watanzania tukiamua tutafanikiwa” -Rais Magufuli
Ameitimisha kwa kushukuru “Nashukuru sana Mzee Mengi kwa kunialika, nimekuja kwa heshima kubwa sana kwako, lakini pia wewe ni mlipa kodi mzuri sana ndomana nimekuja” -Rais Magufuli
LIVE: Rais Magufuli kwenye uzinduzi wa Kitabu cha Mzee Mengi