Spika wa Bunge Job Ndugai amezipokea habari za kwamba kuna baadhi ya Wabunge wametajwa kuhusika kuwatelekeza watoto wao ambapo amelieleza Bunge kuwa wote waliotelekezewa watoto hao wanaweza kumuona ili ashughulikie suala hilo.
“Kuna zoezi linaendelea huko Dar es salaam sasa kidogo kiti cha Spika kimetikiswa hivi… tunatuhumiwa mahali kidogo, natarajia kupata ushauri wenu kama tunafanyaje katika hili maana kuna watoto wetu wapo barabarani na lazima tujue ni nini cha kufanya”
MAJIBU: Kuhusu nembo ya Taifa kuwa na Mwanamke alievaa ‘wigi’