Tabasamu muruwa linaendelea kuchanua na kupamba nyuso za Watanzania mbalimbali ambao wanatembelea Banda la Vodacom Tanzania kwenye Maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ‘Sabasaba’ wakionesha kufurahishwa na kujiunga na huduma mpya ya “RED RLX”.
RED RLX ni moja ya huduma miongoni mwa huduma nyingi zinatolewa na Vodacom Tanzania ambayo inashiriki Maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara, maarufu kama Maonesho ya Sabasaba ambaoo mamia ya Wateja wamekuwa wakifurahishwa nazo.
Unaambiwa Huduma hii ni mpango unaojumuisha vifurushi na kulipa kadri mteja anavyotumia kwa lengo la kuwafanya wateja wake waishi bila wasiwasi inapokuja issue ya mawasiliano kwa kupata dakika nyingi, MB za internet nyingi, SMS nyingi na dakika za kupiga simu nje ya nchi.
Mteja wa Vodacom anaponunua bando ya RED, hupata kipaumbele katika kuhudumiwa bila kupanga foleni anapotembelea duka lolote la kampuni hiyo na atapata huduma ya SOKONI App BURE pamoja na taarifa fupi ya M-Pesa BURE pindi anapohitaji na huduma ya kipekee pindi atakapowasiliana na huduma kwa wateja.
Naambiwa pia RED inatoa vifurushi kama: Silver kwa Tsh. 30,000 ambapo unapata dakika 600 (mitandao yote), 3GB za Data na SMS 3,000 huku kifurushi cha Gold kinakupa dakika 1,000 (mitandao yote), 7 GB za Data na SMS 7,000 kwa Tsh. 50,000. Kifurushi cha Platinum ambacho ni Tsh. 95,000 kinakupa dakika 2,500 (mitandao yote), dakika 30 (Kimataifa), 20 GB za Data na SMS 15,000.