Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika club ya KRC Genk Mbwana Samatta, leo jina lake limerudi kwenye headlines za usajili tena.
Mbwana Samatta leo kupitia mitandao mbalimbali ya habari za michezo Ulaya zimeripoti kuwindwa kwa staa huyo na vilabu vya Ligi Kuu England ili ajiunge nao katika dirisha la usajili la January.
Samatta hadi sasa ameripotiwa kuhitajika na vilabu vya Burnley, Everton, West Ham United na Brighton zinazoshiriki Ligi Kuu England, Samatta ameonesha uwezo mkubwa akiwa na Genk msimu huu akicheza game 16 za mashindano yote na kufunga jumla ya magoli 14.
Kama Samatta akifanikiwa kusajiliwa na vilabu kimoja kati hivyo vya EPL, atakuwa anapata fursa ya kucheza Ligi moja na mastaa wakubwa kama Eden Hazard wa Chelsea, Paul Pogba wa Man United na Sergio Aguero wa Man City, hata hivyo Samatta amewahi kuripotiwa kuwindwa na Levante ya Ligi Kuu Hispania.